Translate

Tuesday, March 26, 2019

NAMNA YA KUMFURAHISHA MPENZI WAKO


 NAMNA YA KUMFURAHISHA MPENZI WAKO



Na SIXBERTY MANSON







Kumpenda mtu ni rahisi lakini kwa kuishi huo upendo, yaweza kuwa ngumu kidogo. Ian Isherwood anasema kuwa kurudiarudia huu mshororo wenye maneno matatu tu, "I Love You" Mara kwa mara haitoshi kuweka mapenzi ya uhusiano wenu kunoga zaidi milele. Kuna Sentensi sita muhimu sana ukimwambia mpenzio mara kwa mara napenzi yenu yafikia upeo.

Kila mtu ana njia yake ya kumwonyesha mpenzi wake kuwa anampenda na kumjali. Haijalishi ni maneno yepi hutumia. La maana ni kwamba uhusiano wake na mpenziwe unadumu kwa raha tele.

Ukitumia maneno mazuri kwa mpenzi wako unampa furaha na kumwonyesha kuwa yeye ndiye mtu wa kipekee kwako duniani. Kama unaye mpenzi, anza kutumia , maneno haya sita na uhusiano wako utakuwa wenye raha; 

1. Nimebahatika kuwa nawe 

Kumwelezea mpenzio vile unajisikia kubahatika kuwa naye katika maisha yako ina uzito zaidi kuliko " Love You".

Wakati unampenda mtu sana unajiona duni kwamba hata kuona amekufanyia fadhila ({Favour) kuwa nawe. Yaani ni kama huna cha kumrudishia kama shukrani kwa upendo wake kwako. Ukisema haya wamfanya kujiskia amependwa na kwamba unafurahia anayokufanyia. 


2. Pole/ Samahani 

Kusema Pole baada ya kukoseana au majibizano madogo huongeza mapenzi katika ndoa yenu. Kusema "pole" haitamaanishe eti wewe ni hafifu sana kumliko mwenzio. Kila ndoa huwa na majibizano, wivu na kutoelewana. Lakini baada ya hayo yote, sema "pole" na kwa ukweli yatapoa! 

3. Nimekusamehe 

Ni vigumu kwa mtu kuomba msamaha lakini ni vigumu zaidi kusamehe mtu. Msamaha ni jambo muhimu sana katika uhusiano. 

Ni ngumu sana kuifanya mara kwa mara lakini ndiyo huongoza na kupeana mwelekeo wa ndoa. Haina haja kushikilia mabaya ili kuharibu ndoa yako. Msamehe tu!

 4. Nipo hapa kwa ajili yako 


Ukimpenda mtu, mkubali kwa jiinsi alivyo kwa uzuri au ubaya. Hakuna aliyekamilika. Wakati mwenzako anapitia magumu, hakuna maneno yanayompa nguvu kuliko " Nipo hapa kwa ajili yako" kutoka kwa ampendaye. Maneno haya humhakikishia mwenzio kuwa una yeye katika hali zote za kimaisha. 

5. Nakuamini 

Bila kuaminiana ndoa haiwezi dumu. Ndoa hupata majaribu hata ikiwa ya miaka hamsini! Lakini la muhimu sana ili kudumisha mapenzi katika ndoa ni uaminifu. Habari Nyingine: Inashangaza: Mume amuuza mkewe kwa mtalii! Ukimwambia mwenzako unamuamini, basi umeondoa hisia za mbaya kumhusu kama wivu ambao ni hatari sana kwa ndoa. 

6. Nijitolea kwako kikamilifu 


Kujitolea kwa hakika kwa mpenzio huonyesha kuwa ulimchagua yeye pekee, kawa mwaminifu na kampeda kwa dhati. Kila mtu hutaka kuhakikishiwa kuwa ni yeye tu katika uhusiano. Usione ni kawaida kuwa na mpenzio. 



NB
Some people use these words with malicious intent. If you persuade a participant to either benefit yourself financially. Don't be deceived! see also their actions if they are in line with their words. 



















No comments:

Post a Comment

SIXBERTY MANSON POSTS

Mona Lisa

  MONALISA                              LA GIOCONDA                          By Sixberty Manson  A picture by Sixberty Manson  MEET THE REAL...

ZILIZOTAZAMWA ZAIDI