FREEMASON AND THE DEVILS TRIANGLE
Part One.
By sixberty manson.
Umasoni ni chama cha siri kabisa cha Kiyahudi, kimeanzishwa huko enzi za Kiroma sehemu za Aurshalim (Jerusalem) wakati wa ufalme wa Herodus Aghriba baina ya mwaka 37-44 M, aliyekuwa mjukuu wa Herodus Mkuu, muuaji wa watoto wa Bethlehem kwa khofu ya kutokea Yesu, ambaye kwa mujibu wa imani zake, aliazimia kuondosha haraka iwezekanavyo utawala wote wa Herodus.
Umasoni ulitambulika kwa utata wake na mtindo wake ulio na amri madhubuti. Malengo yake ni kuhakikisha mamlaka yanabaki kwa Mayahudi duniani kote. Unahubiri upagani, utenganifu wa jamii na upotofu. Jumuiya hii inachagua wajumbe wake miongoni mwa watu maarufu kwenye nyanja ambazo zina nafasi kisiasa, kiuchumi au kijamii. Kitabu cha Simplified Encyclopedia kimeandika na kuchapisha kutoka WAMY (Baraza La Vijana Waislamu Duniani - World Assembly of Muslim Youth – Saudi Arabia) kinafafanua kwamba muasisi wa jumuiya hii ni Herdous Aghriba (44 M) mfalme wa Kiroma kwa msaada wa wasaidizi wa Kiyahudi.
Hivyo, mwanzo wake ulitokana na ujanja, hila na mageuzi. Inachagua zana za utambulisho, majina na alama ili kueneza khofu na kuwafanya watu kuamini katika habari zisizo sahihi. Rabai Laquiz amesema: “Umasoni ni ya Kiyahudi kwa mujibu wa historia yake, uongozi wake, mafundisho yake, zana zake za siri na kazi zake za ubunifu wa hali ya juu... Ni ya Kiyahudi kuanzia utosini hadi miguuni. Ilikuwa ikiitwa: ‘Uwezo wa siri wenye lengo la kuwaadhibu Wakristo, kuwauwa viongozi, kuwakata vichwa, kuwapiga pande na kuizuia dini yao kuenea.’ Sasa, imechukua jina hili (Umasoni – Freemasonry) kwa kipindi cha karne kadhaa”.
Neno “mason” lina maana ya yule mwenye kujenga nyumba. Hivyo “Free masons” lina maana ya Wamasoni walio huru. Hii ndio ilikuwa haswa alama yao wakati walipokuwa wakifanya kazi zao (za kujenga nyumba). Lakini sasa jina hilo lipo mbali na tafsiri hii. Enzi hizo ndio zilikuwa mwanzo wa umoja huu. Lakini vitu vilianzia tokea 177 M pale Adam Webshawit, Mkristo aliyeingia kwenye upagani, alipovutiwa na umoja huu ambao alidhani utamsaidia kuimiliki dunia yote.
Mara ya mwisho kutimu kazi hii ilikuwa ni mwaka 1776 M, na bodi ya mwanzo kuanzishwa ndani ya kipindi hicho (Bodi ya Torani) ilipewa jina baada ya huyo Shetani wao waliokuwa wakimwabudia. Ukweli ni kwamba, Webshawit alikuwa ni mtu wa mwanzo aliyeanzisha mipango ile ile ya Umasoni.
Azma ya mwanzo ya Umasoni ni kuupiga vita “Ukristo”. Baadaye, azma zao ziliendelea kupiga vita dini zote, kuirudisha tena Israel na kuitoa Palestine.
Malengo muhimu na imani zao kuu za wajumbe wa jumuiya hii ni:
1. Wanaitakidi kwamba imani kwa Allaah, Mitume na Vitabu kama ni upuuzi na hawaamini chochote katika ghayb.
2. Wanashiriki kwa hali zote kubadili serikali ili kuweka serikali ambayo inawakubali wao pamoja na mawazo yao.
3. Wanahubiri ukombozi wa ngono na kumuona mwanamke kama ni aina fulani ya umiliki.
4. Wanafanya bidii kuchana chana mataifa – isipokuwa taifa la Kiyahudi na kuanzisha migongano ya kudumu baina yao.
5. Wanauza na kutoa silaha kwa pande zote mbili ili kushinikiza mapigano.
6. Wanafanya kila jitihada ya kuendeleza ukabila na uadui.
7. Inaua na kuharibu kanuni za maadili kwa kutumia hongo kupitia ngono na pesa ili kuwavutia wenye kutoa maamuzi.
8. Wanafanya uchunguzi wa kudumu (na kuzifanyia kazi) ili kuwazuia Waislamu na kuwapunguza kupitia aina zote (birth control) na kongamano zinazoshajiisha mambo hayo kama vile: “Kongomano La Wazawa”.
Mwaka 1717 M, Umasoni ulijitokeza kwa jina jengine jipya: Jamii ya Kimasoni (Freemasonic Society) au Wamasoni (Freemasons), wakitekeleza malengo yake ya kupiga vita dini zote. Pia walichukua nembo mpya: Pembe tatu baadaye ikagaiwa (pande mbili), baadaye walianzisha kituo chao cha mwanzo cha Kimasoni nchini Uingereza, wakiwa na kauli mbiu mpya: uhuru, udugu na usawa. Baada ya hapo, walitoa maamuzi ya kuweka (wazi) maazimio yao ya kweli kama ifuatavyo:
1) Kuuendeleza Uyahudi.
2) Kupiga vita dini zote, haswa Ukatoliki.
3) Kueneza ukafiri na ukombozi.
Baadaye, vituo vipya na vingi zaidi vilifunguliwa ndani ya Marekani. Waislamu wengi mno walidanganyika na kauli mbiu ya Umasoni, kisha wakaungana nayo. Lakini, walipotambua malengo yake sahihi, walinawa mikono yao na kuondokana nayo. Wengi wa walioachana na amri hiyo, walikataa kuweka wazi siri zake wakikhofia kuuawa. Utafiti mwingi uliofanywa na waandishi wa Magharibi na magazeti ya Kiyahudi pamoja na chunguzi za nyanja makhsusi, zilidhihirisha kwamba Wayahudi wamekuwa wakipanga kuuharibu ulimwengu kupitia “wito wa kutia shime ulio imara” ambao Waislamu ni lazima wauelewe. Kauli mbiu yao maarufu inasema: ‘Dini zinatusababisha kugawana wakati Umasoni inatupeleka kwenye umoja’. Imesimuliwa ndani ya Kitabu cha Masonic Encyclopedia kilichotolewa Phila mwaka 1906 M kwamba kila kituo cha Kimasoni kiwe na nembo ya kudhihirisha sinagogi la Kiyahudi, (na ukweli ni kwamba) kila mwalimu lazima awe mwakilishi wa mfalme wa Kiyahudi na kila mtu wa Umasoni amuajiri mfanyakazi wa Kiyahudi.
Ifuatayo ni nukuu kutoka gazeti la Masonic lililotolewa huko London mwaka 1935 M: ‘Shabaha yetu ni kuunganisha amri ambayo wanachama wake watatekeleza mahusiano ya kingono’. Hivyo, walianzisha maeneo (clubs) ambayo watu walitembea utupu na walifanya kila waliwezalo kuharibu thamani ya maadili.
Ili kutimiza malengo yao hapo juu, Wamasoni walianza kutumia majina tofauti kama vile Wana Wa Agano – Children Of Covenant, Kiwanis, Lioness, Yahweh Presence, Exchange, Rotary clubs na nyenginezo.
1) Wana Wa Agano. Kundi hili la Kimasoni lilianzishwa New York mwaka 1843 M; wanachama wake walikuwa ni Wayahudi tu. Baadaye, lilipanua matawi yake duniani kote. Foster Dallas akiwa kwenye mkutano ulioitishwa na kundi lake mnamo tarehe 03/05/1966 M alisema: ‘Ustaarabu wa Kimagharibi unatokana na Imani za Kiyahudi, nchi zote za Magharibi ni lazima zitetee ngome ngumu ya Ustaarabu wao: Israel’.
2) Kiwani. ‘Jitambue mwenyewe namna ya kuifanya sauti yako isikike’ Kundi hili lilipewa leseni ya kuanzishwa kwake mwaka 1915 M huko Detroit, USA.
3) Lioness. Kundi hili lilijitokeza Chicago, Chicago ambayo ndio ardhi mama ya vyama vyote vya Rotary. Kwa mujibu wa makala ya al-Ahram ya tarehe 02/12/1985 M. Mkuu (wa kike) wa kuiwekea dhamana na harakati za kijamii alifungua klabu ya mwanzo ya Lioness Nambari 19 huko Misri – Cairo, ni klabu ya kisasa kuliko zote. Saini na vyeti vilikabidhiwa katika maadhimisho ya (kuvipatia usajili) Vilabu 27. Majina ya makada wa chama hichi yalitajwa ndani ya makala hiyo.
4) Exchange. Ilianzishwa Detroit nchini USA mnamo tarehe 27/03/1916 M kutokana na nguvu za “Charles Berki” tajiri wa vito (vya dhahabu, almasi na kadhalika); aliitisha mkutano wake wa mwanzo mwaka 1917 M.
5) Yahweh Presence. Ni msingi wa Kiyahudi katika mavazi ya Kikristo. Yahweh ni agano binafsi la jina la Mungu (Agano la Kale); lililoanzishwa huko Penn. USA mwaka 1884 M, na baadaye, kuhamia New York mwaka 1909 M. Kundi hili linawatembelea watu majumbani mwao ili kuwahamasisha kuziimarisha kanuni zao zilizoegemezwa kwenye Taurati (na zilizoingizwa uongo kwa mikono yao). Kundi hili ni la hatari zaidi miongoni mwa Jumuiya za Kiyahudi, kwa vile linadanganya wanaharakati (wapo tayari hata kuua) wa Kikristo na kupandikiza ndani ya akili zao dhana za uongo za utume kama vile Ardhi Iliyoahidiwa Promised Land.
Pia, ofisa wa Kimarekani alitoboa siri zao ndani ya kitabu chake ‘Dunia Ni Doli La Kiizraili’; kilichotafsiriwa kwa Kiarabu.
Hapa, ni vyema kutaja baadhi ya vitabu vilivyoandikwa kuhusu Umasoni. Dr. Muhammad Ali az-Zu’bi ameandika al-Masuuniya Fil ‘Aaraa (Umasoni Ndani ya Hewa Wazi) na Ahjar kwenye Riqat ash-Shataranj (Kitunda Katika Mchezo Wa Sataranji – Pawns On The Chess). Dr. Muhammad alikuwa ni mfano hai wa wasifu wa Kimasoni nchini Lebanon. Baadaye, alitubia na kurudi kwenye Uislamu. Hivyo, amri za Kimasoni ziliamuru auawe.
Zifuatazo ni Fatwa za Kishari’ah kuhusiana na Umasoni na wanachama wake zilizotolewa na Baraza la Fiqhi kwenye kikao chake cha kwanza kilichofanyika Makkah mnamo tarehe 10/08/1398 H. sawa na tarehe 15/07/1978 M.
Baada ya kusoma na kuchunguza yale yote yaliyoandikwa na kuchapishwa kuhusiana na amri hii, Baraza linatoa Fatwa kama ifuatavyo:
1) Umasoni ni amri ya siri, yenye kanuni na mafanikio ya siri; hakuna mtu anayetambua siri zake hata kwa wajumbe wake walio wengi, isipokuwa wale wenye vyeo vya juu. Mara nyingine wanafanya kazi ndani ya jamii.
2) Inajenga uhusiano wake miongoni mwa wajumbe wake duniani kote kwa njia za mahusiano ya kidugu ya uongo kwa lengo la kuyaweka mafanikio yake siri; inahusisha dini zote na imani zote.
3) Inavutia watu kujumuika nao kwenye jumuiya zake kwa kutosheleza matakwa yao binafsi, kwa vile kila Mmasoni ni lazima amtumikie ndugu yake duniani, yaani kumsaidia kutimiza ndoto zake zozote zinavyokuwa na kumsaidia kutatua matatizo yake na kumtimizia mafanikio yake na malengo yake; wanafanya kazi mmoja kwa mwengine kwenye mazuri na mabaya, haki na dhulma hata kama watajitahidi wawezavyo kujionesha kwamba wanafanya hayo kwa msaada mwema. Kwa maneno mengine, amri za Kimasoni zinafanya kazi kwa matakwa ya wajumbe wake ili kupata nafasi za mbele kwenye jamii na hilo ni miongoni mwa vivutio vyao. Wajumbe wake wanasaidia michango muhimu.
4) Kujiunga kwa amri hii kunaanzia kwa sherehe za kimila zinazoonesha matendo ya kutia khofu ili kumtisha mjumbe iwapo atakiuka mafundisho yake na amri zake na wakubwa wake.
5) Wajumbe wengine kutokana na umuhimu/ nafasi zao wanaruhusiwa kufuata mila za dini zao, lakini wanaamriwa kufanya baadhi ya maagizo kwa mujibu wa uwezo wao na wanatayarishwa kuwa ni mapagani (asiyesadiki mungu) pamoja na kushika nafasi za juu kwa mujibu wa huduma zinazotolewa kwa mafanikio na mipango ya hatari.
6) Umasoni una shabaha za kisiasa na kanuni yake ya msingi imo ndani ya vikundi visivyo rasmi na vyenye kutumia nguvu ya kung’oa uongozi duniani kote (coups d’etat).
7) Kimsingi, ni amri siri ya Kiyahudi na Kizayuni.
8) Ndani ya shabaha zake za siri, ni kupiga vita dini zote, haswa Uislamu.
9) Umasoni unachagua wajumbe wake kutoka watu walio hodari kiakili, matajiri, wanasayansi na kwenye kila nyanja ili kutawala kimabavu jamii zote kwa manufaa ya shabaha zake na wajumbe wake.
10) Inabadilisha majina na sifa tofauti, na inafanya kazi chini ya shughuli tofauti haswa pale penye aina yoyote ya upinzani kwa Umasoni ndani ya jamii. Baadhi ya majina yake ni: Rotary, Lioness, na amri za Lions...
Inakuja wazi kwamba Umasoni una uhusiano thabiti ambao unasaidia kutawala na kuongoza wengi walio madarakani ndani ya Palestina. Inatoa amri duniani kote na baadaye inachukua matunda kutokana na hali hiyo.
Kwa kuegemea ukweli ulioelezwa hapo nyuma kuhusu shabaha mbovu na za hatari zinazotumiwa na Umasoni, Baraza la Fiqhi linaamini kwamba amri kama hiyo ni yenye kuleta uharibifu, kwani inapigana vita dhidi ya Uislamu na Waislamu na kila mtu anayejiunga nayo ni kafiri.
No comments:
Post a Comment