HADITHI YA KUSISIMUA
HADITHI HII IMETUNGWA NA SIXBERTY MANSON ..KUTOKANA NA MVUTO WAKE NIMEIWEKA HAPA KWA NIA YA KUPATA BURUDANI KWA WAPENZI WA HADITHI KAMA MIMI..................................................................................................................
Tangu utotoni nilijuwa kuwa nimejaliwa uzuri wa maumbile na sura. Nikiwa mtoto wa kike wa pekee na wa mwisho wa Mzee Erasto Malyamkono (mtaani alijulikana kama Mzee Mswahili) nilikuwa nimedekezwa nikadekeka. Kaka zangu walikuwa wakinichunga utadhani mboni ya jicho vile, na hakuna kitu nilichotamani ambacho sikukipata. Nilijitahidi kuitunza heshima yangu na heshima ya familia hususan maswala ya wanaume. Nilimaliza kidato cha nne kule Bwiru Mwanza na baadaye kujiunga na shule ya Masista wa Damu Takatifu kule Kifungilo Lushoto. Hadi naanza kidato cha tano nilikuwa bado bikira.
Kabla ya hapo vijana wengi kule mtaani maeneo ya Isamilo walikuwa wakinitaka na kunifukuzia. Nawakumbuka kina Maiko, John, Almasi na Mugisha (alikuwa na umbo kubwa na kakichwa kidogo, utadhani hana shingo) wa pale magorofa ya Benki jinsi walivyokuwa wakinisarandia. Nilikuwa mcheshi na sikuwa na maringo yoyote. Yangu yalikuwa ni maneno na ahadi kem kem, lakini kuwavulia chupi la!! Nilikula vi pesa vyao vya sangara n(a kujinoma kwa tuzawadi twao.) Mademu wengi pale mtaani walinichukia sana, na hawakuficha wivu wao. Wengi waliokuwa wakinitaka walikuwa ni watoto wa wakubwa (miongoni mwao walikuwemo mtoto wa Jaji maarufu na mwingine alikuwa ni mtoto wa RPC). Namkumbuka mhindi mmoja ambaye naye alikuwa akinifukuzia ile mbaya. Nilijiona mimi ni malkia wa mbingu nikiitetemesha nchi kila nipitapo.
Ilikuwa ni huko Lushoto ndiko nilikopata kwa mara ya kwanza kuonja joto la mapenzi. Ilikuwa ni likizo ya pili ndipo nilipokutana na Petro J Shekitondo (Alipenda kuitwa PJ). Basi letu lilisimama pale Mombo kwa ajili ya kujipatia chakula kabla ya kuendelea na safari yetu hadi Moshi. Yeye alikuwa ni mfanyakazi katika Hoteli ya Usambara, mojawapo ya hoteli mashuhuri pale Mombo. Nilikuwa nimekaa kwenye meza moja na marafiki zangu wawili; Sakina Mwanakibili (mtoto wa Mbunge) na Grace Chambi (mtoto wa Katibu wa Wizara, ambaye boyfriend wake alikuwa Mbunge mmoja).
Tukiwa tunapeana gumzo, tulikatishwa mazungumzo yetu na kijana mrefu, aliyevalia suruali ya jeans na T-Shirt yenye maandishi ya “Daytona Beach” Kifuani. Alikuwa ni mtanashati na sote watatu tulijikuta tukipoteza mtiririko wa mawazo kwa sekunde.
“Habari zenu” Alitusalimia kwa sauti nzito yenye upole
“Powa” Tulimjibu kwa pamoja huku tukijifanya hatumjali “Mko tayari kuagiza chochote” Alituuliza tena akituangalia kwa kutupokeza.
“Tupe dakika chache” Nilisema kwa niaba ya wenzangu, ambao waliafiki kwani muda wote huo tulikuwa tukipiga gumzo wala hatukuaangalia ile menu ubaoni.
“Clara” Grace aliniita
“Nini” Nilimjibu
“Mbona unamuangalia kaka wa watu utadhani unataka kummeza!” Aliniambia
“Hamna kitu, nilikuwa mbali tu” Nilimjibu, laiti wangejua ni umbali gani nilikuwa!!
“aha!” Walihamaki wote wawili kana kwamba hawakuamini maneno yangu. Aliporudi tena alijitambulisha kwetu kwa jina na kuchukua oda zetu.
Tulikula kwa haraka haraka kwani tulianza kusikia honi ya basi letu ikianza kulia. Kama kawaida tuliangalia alipokaa dereva na demu mmoja wakila, hatukuwa na haraka. Tulipomaliza kula tulijiandaa kuondoka. Kabla hata hatujafika nje tukasikia mtu akituita.
“Samahani kina dada” Alikuwa ni PJ Shekitondo.
“Nini tena” Tulimuuliza tukishangaa labda tumesahau kitu.
“Dada wewe” akinionyesha mimi, “naomba nikuulize kitu” alisema. Tukasogea chemba. Akaja karibu yangu kiasi cha kusikia joto la mwili wake na akasogea kuninong’oneza jambo.
“Tangu uingie hapa hotelini macho yangu yalikuwa kwako, natamani tufahamiane” Aliniambia na sauti kakamavu ilivunja vunja kila vizuio nilivyokuwa navyo. Sikuamini kuwa mwanamme anaweza kunigusa kihisia namna hiyo.
“Mbona basi letu liko karibu kuondoka” Nilimjibu kwa aibu na kudengua kidogo
“Si unasoma Kifungilo” Alinijibu kumbe alishajua mimi ni Mwanafunzi.
“Umejuaje? Kwani tuna alama kwenye paji?” Nilimjibu kwa aibu.
“Nimeshawahi kukuona mlipokuja Mazinde Juu kwa debate” Alinijibu. Dereva wa basi alitoka nje na kuelekea kwenye basi. Nikajua nilazime niamue haraka.
“Sikiliza John” Nilimwambia, “Ninarudi tena shuleni mwezi ujao katikati, labda tuwasiliane wakati huo au vipi?” Nilimwambia.
“Poa tu” Alinijibu.
Alichukua kipande cha karatasi na kuandika namba yake ya simu na kuniambia kuwa siku nikiwa njiani kurudi nimpigie ili tukutane. Nilimwahidi kuwa nitampigia simu wakati nikirudi toka likizo. Nilikimbilia kupanda basi. Rafiki zangu waliniangalia kwa mshangao jinsi uso wangu ulivyong’ara kwa aibu na soni. Wakataka niwasimulie yaliyotokea. Nilisubiri kwa hamu siku ya kurudi toka likizo.
***
Jinsi nilivyongojea kwa hamu likizo iishe. Nilikuwa najisomea vitabu, kuangalia TVs (hasa Oprah) na MTV n.k. Hata hivyo mawazo yangu yalikuwa kwa PJ tu. Sijui itakuwaje nikimuona, sijui bado atanionyesha kunitaka... nilifikiri nguo nitakazovaa na kama niweke nywele rasta au kalikiti. Kwa uchafu wangu wa mawazo nimwazia akiwa uchi mbele yangu!!, je nanihi yake kubwa kiasi gani!! Sijui niiguse au la. Mara nyingi nilijikuta nikijichekea mwenyewe. Katika hayo yote ilibidi nikubali mwenyewe kuwa sikuwa na utaalamu katika fani hiyo. Sijawahi kufanya mapenzi na mwanamume yeyote. Nilihisi kutetemeka kwani labda PJ anafikiri mimi nimeshawahi kuwa na mwanamume na hivyo atatarajia nimwonyeshe vitu vya nguvu kitandani. Itakuwaje basi nikiboronga? Nikatamani siku za zamani ambapo mabinti walikuwa wanakwenda unyago na kufunzwa na kufundwa!! Sijui nianzie wapi, nilijiwazia. Niseme wazi kuwa mambo mengi ya mapenzi nilijifunza toka gazeti la “Heko” kwenye darasa lake la Mapenzi na vitabu vingi vya mapenzi. Hata hivyo niligundua kuwa hakuna kitu mbadala zaidi ya kujifunza kwa vitendo. Nikaamua kuwa nitaenda kumwona dada Bupe.
Bupe alikuwa ni miongoni mwa kina dada waliochangamkia biashara ya mapenzi. Nilitambulishwa kwake na wanafunzi wenzangu wakati tukisoma Bwiru. Baadhi ya wanafunzi wa Bwiru walikuwa wanaunganishwa na Bupe na vibosile wa Mwanza na walikuwa wakikutana nyumbani kwa da Bupe pale Pasiansi si mbali sana na ule uwanja wa ndege wa Mwanza. Dada Bupe alikuwa ni kama anawamiliki wasichana hao. Kila mwisho wa wiki tunapopata ruhusa ya kwenda mjini, wengi walikuwa wanaishia kwa Bupe. Nilipopewa nafasi hiyo mimi nilikataa na sikurudi tena. Lakini nikimuwazia PJ nikagundua kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kunisaidia zaidi ya dada Bupe. Nilifunga safari siku ya Alhamisi na kupanda vi- Express yaani daladala za Mwanza hadi Pasiansi. Kwa vile ilikuwa ni wakati wa likizo, sikutarajia kukuta “wageni wengi pale”. Kulikuwapo na gari moja Toyota lenye nembo ya “Jimbo Kuu la Mwanza” limeegeshwa uani. Nilipobisha hodi, si mwingine aliyefungua mlango ila dada Bupe. Sikutaka kujua gari la Jimbo linafanya nini kwa kungwi.
“Karibu, nikusaidie nini?” Alijibu bila kuonyesha kama ananikumbua au la.
“Shikamoo da Bupe” Nilimsalimu nikipiga goti langu kidogo kwa mtindo wa Kisukuma.
“We acha kunizeesha, mambo vipi?” Badala ya kuitikia “marahaba” aliniyeyushia kiaina. Siku hiyo alikuwa amevalia kaptula ya khaki iliyomkaa vyema na alivalia T-shirt ya rangi nyekundu yenye maandishi ya kumetameta yasemayo “Playgirl”.
“Hunikumbuki, da Bupe” nilimuuliza. Tulikuwa bado tumesimama mlangoni.
“Nikumbushe basi usiniambie wewe ni ndugu yangu” Alisema akicheka.
Nilimkumbusha jinsi nilivyokutana naye kwa mara ya kwanza wakati nikisoma Bwiru kama miaka michache tu iliyopita. Akataka kujua kilichonileta hapo kwake, nilimweleza kinaganaga jinsi nilivyojikuta niko njia panda. Nilimuomba msaada wa ushauri wake. Akanikaribisha ndani, kwenye sebule iliyopambwa vizuri kwa makochi ya kifahari na samani za kila aina.
“Yaani unataka nikufundishe kufanya mapenzi” Aliniuliza
“Ndiyo, na zaidi jinsi ya kumridhisha mwanamme” Nilimwambia
“Ok, nitakufundisha itakugharimu lakini” Aliniambia
“Shilingi ngapi?” Nilimuuliza
“Shilingi eflu ishirini tu” Aliniambia bila hata ya kupoteza pumzi. Nilikubali.
Akaniambia kuwa nirudi na hizo fedha kesho yake, na niwe tayari kwa somo la kwanza litakalohusisha mimi kuvunjwa bikira yangu. Nilirudi nyumbani nikijisia afueni lakini mwenye wasiwasi. Sikujua kama uamuzi wangu ulikuwa ni wa busara au la. Hata hivyo nikajisemea moyoni, “maji ukiyavulia nguo, huna budo uyaoge”. Nimeyavulia nguo, niko tayari kuyaoga.
Itaendelea......
No comments:
Post a Comment