Translate

Friday, June 19, 2020

ENEMY KILLED IN ACTION (sixberty manson)

OPERATION GERONIMO EKIAENEMY KILLED IN ACTION)



Na: Sixberty manson 

OPERATION GERONIMO EKIA" (EKIA - Enemy Killed In Action "Adui ameuawa kwenye mapambano") NI OPERATION ILIYO RATIBU NA KUFANIKISHA KIFO CHA OSAMA BIN LADEN.

Neno "Geronimo" linatokana na lugha ya Apache ambao asili yao ni jamii ya Wahindi wekundu (Red Indian),lakini katika mkakati ulio ratibiwa na jeshi la Marekani katika mission ya kumuua Osama Bin Laden neno hii ilitumika katika kutekeleza operation maalumu ya mauaji ya Osama bin Laden iliyo pesa jina "Operation Geronimo EKIA" (adui aliuawa katika mapambano) 

Matumizi ya neno Geronimo ulianza kutumika nchini Marekani toka kale, hasa ukirejea katika simulizi za mwanamama aliyeitwa Geronimo, Yeah jina hilo ni jina la mtu ambae alikuwa ni kiongozi na mlinzi wa ardhi ya kabila la "Apache" na shujaa wa Kiamerika dhidi ya uvamizi wa wazungu katika eneo lao (America).

Hadithi na simulizi za huyu mwana mama "Geronimo" imeelezewa vizuri na bwana Ben Zimmer, ambaye ni mwanahistoria na mtafiti wa makabila ya asili ya huko Amerika (native American), mwana historia huyu alichunguza asili ya neno hilo na historia nzima ya mpiganaji huyo kutoka kabila la Apache, ambapo baadae Zimmer aligundua kwamba neno hilo lilimanisha "ngoma ya mvua," "njia ya vita," au "rangi ya vita" na neno hilo linatokana na desturi ya asili ya Waamerika yani "Waapache".

Hii operation ya "Geronimo EKIA" ni moja ya OPERATATION kubwa na ndefu ndani ya taifa la Marekani na shirika la kijasusi la CIA, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya ulizi ya Marekani (The Pentagon) inasema kuwa operation hii ni muhimu katika historia ya taifa la Marekani, kwani operation hii ni operation kubwa nchini kuliko operation yoyote ile ya taifa hilo.

Taarifa za wizara hiyo zilizotolewa mwaka 2014 na wizara ya ulinzi ya Marekani (US National Security Statistics Bureau) zinaiweka operation Geronimo EKIA kuwa operation kubwa na bora zaidi duniani ambayo iliigharimu serikali ya Marekani $1.4 trillion dollars (fedha hizo ni sawa na pato ghafi la uchumi wa Spain).

Kutokana na takwimu hii inaifanya Operation Geronimo kuwa Operation hatari na muhimu zaidi kati ya operation zilizowahi kuratibiwa na taifa hilo, operation hiyo ambayo ilimrenga kumkamata Osama Bin Laden, mtu ambae taifa la Marekani linamtaja kama mtu hatari sana kwenye historia ya usalama wa taifa hilo katika karne ya 20.

Operation Geronimo EKIA Inatajwa kutumia gharama kubwa kutokana na kuhusisha operation zingine ndogo nne, ambazo ni "Operation Convet", "Operation Neptune spear", "Operation Dr Shakir Vaccination" na "Operation Abbottabad" Operation hizi zote nne zilifanyika chini ya Operation Geronimo EKIA.

Pamoja ya kuwa operation ya hali ya juu na ya kisasa zaidi katika historia za kijasusi duniani kuwahi kufanyika, kwa kuhusishwa na kutumia kitita kirefu cha pesa dunian huku ikifanyika kwa mda mrefu karibu miaka kumi toka 2001-2011 na kwa ujuzi na uhatari mkubwa bado imekuwa ikipingwa na watu wengi hasa wachambuzi wakubwa duniani.

Kupingwa kwake kunatokana na kughubikwa na usiri wa hali ya juu kuhusu kifo cha Osama Bin Laden, kwa mujibu wa operation hiyo inaoneshana kwamba Osama Bin Laden alikamatwa na kuuwawa lakini hakuna ushahidi wowote ule wa mwili wake au vipimo vya DNA (vinasaba) vyake. 

Nje ya hilo wakosoaji wake husema Osama Bin Laden akuuwawa na Marekani kutokana na uhalisia kuwa mdogo katika kuhusisha kifo cha Osama Bin Laden na yule aliyedaiwa kuuwawa katika usiku ule wa kuamkia tarehe 1 may 2011.

Usiku huo wa kuamkia tarehe 1, May 2011 siku ambayo ndio ilikuwa mwisho wa Osama Bin Laden. Bado inautata kwakuwa hakuna mtu yoyote yule ambae aliyeuona mwili wake. Inadaiwa kuwa alizikwa kwa heshima baharini kwa kuzingatia imani ya 


Lakini nani wa kuamini hilo? Hata kuamini kama aliuawa kweli ni hadi mwanaye Hamza Bin Osama Bin Laden na kundi la Al-Qaeda walipothibitisha kifo cha Osama Bin Laden siku chache baadae japo hilo wachambuzi wengine uliona kama mbinu ya kumficha Osama Bin Laden dhidi ya kuendelea kitafutwa na Marekani.

Nje ya ubora wake na umuhimu wake katika operation zote zilizowahi kufanywa na serikali ya Marekani bado kuna hoja kadhaa ambazo zimekuwa zikiendelea kuifanya operation hii kuwa na maswali mengi katika kufanikiwa kwake.

Pamoja na yote hayo bado operation hii Geronimo EKIA ni muhimu katika historia za operation zote duniani. 

Operation hii iliyopewa jina la "Geronimo EKIA" yani (adui aliuwawa katika mapambano) ambayo ni mission na mkakati mkubwa wa kuuwawa kwa Osama Bin Laden, kwa Tanzania ulisimuliwa kwa mara ya kwanza na Mchambuzi wa maswala ya kijasusi na mwandishi mashuhuri wa sayansi ya upelelezi na mission za kijasusi duniani ndugu Khabibu Anga maarufu kama "The Bold".

The Bold alifanya uchambuzi wa kina na Kusimulia kwa upana Operation hii ya Geronimo EKIA tarehe 12/11/2016 ambayo inapatikana kwenye Jukwaa la JamiiForums kwa jina la *"Geranimo IKEA: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley"* ambayo imekuwa posted Jamiiforum September 12, 2016.

Kwa mujibu wa "The Bold" anaeleza kuwa upatikanaji wa Osama Bin Laden ulianza kupitia "Operation Convet" iliyofanyika katika milima ya Tora bora, katika milima hii taarifa zote za awali zilizo wezesha kupatikana kwa Osama Bin Laden zilianzia hapo. Hivyo kuifanya milima hiyo ya Tora bora kuwa source ya Operation Geronimo EKIA.

Hivyo turejee simulizi hii ya "The Bold" aliyoipa jina la "Geranimo IKEA: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley" ya September 12, 2016, kuona namna Operantion nzima ya Geronimo EKIA ilivyo fanyika ambapo tukio zima lilikuwa hivi.... 

Mwaka 2001, mwezi Desemba katika milima ya Tora Bora baada ya mapambano ya siku kumi na moja toka tarehe 6 hadi 17 na mabomu kadhaa kudondoshwa katika milima hiyo hatimaye askari wa miguu walianza zoezi la kuikagua milima hiyo kuangalia kama kuna masalia yoyote muhimu yanayoweza kuwapa fununu ya kuielewa vita waliyoianzisha kati yao Majeshi ya Marekani na Wanamgambo wa Taliban.

Katika mchakato huo wa ukaguzi wanajeshi wa marekani walifanikiwa kumuokota kijana mmoja wa umri wa mika 21 akiwa hai. Baada ya kumuokota wanajeshi kadhaa wakampakia katika chopa ya kivita na kurudi nae katika kambi ya kijeshi ya Bagram Air Base iliyo nchini Afghanistan.

Baada ya kufika katika kambi ya Bagram wanajeshi wakaanza kumuhoji kijana huyo ajieleze yeye ni nani na alikuwa anafanya nini katika milima ya Tora Bora.

Baada ya kujitambulisha kijana huyo akawaeleza kuwa alikuwa anawinda katika milima hiyo ya Tora Bora na kwa bahati mbaya akajikuta ameingia kwenye eneo ambalo hakujua kuwa kulikuwa na mapigano ya kijeshi. 

Maafisa wote wa kijeshi hawakuamini maelezo haya na waliendelea kumuhoji kwa siku kadhaa lakini yule kijana alishikilia maelezo yake yale yale kuwa alikuwa anawinda milimani.

Baada ya kutokuwepo kwa mafanikio yoyote ya kumuhoji kijana huyu Maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi katika kituo cha Bagram wakawasiliana na maafisa wa CIA waliopo nchini Afghanistan na kuwaeleza juu ya tukio hilo. Maafisa hao wakawashauri kuwa kijana huyo wakabidhiwe wao ili wamuhoji wao kwa kina. 

Siku tatu baadae kijana huyo akakabidhiwa kwa maafisa wa CIA na wao wiki moja baadae wakamsafirisha kutoka Afghanistan mpaka kwenye jela za siri (Black Sites) za CIA zilizopo ulaya katika nchi ya Romania na baadae akaamishiwa jela za siri nchini Poland.

Baada ya kijana huyo kufikishwa huko mahojiano yakaendelea na akaendelea kushikilia msimamo wake kuwa alikuwa anawinda kwenye milima ya Tora Bora. CIA ikaamua kupanua wigo wake zaidi ili wamtambue. Wakachukua alama zake za vidole na kuziingiza katika mfumo wa alama za vidole wa nchi karibia zote za kiarabu lakini wakapata matokeo sifuri, hakukuwa na taarifa zozote zinazoshabihiana alama za vidole za kijana huyo. 

Hii ilikuwa na maana nyingi lakini maana moja kubwa ni kwamba kijana huyu hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu katika maisha yake, alikuwa ni 'raia mwema'!

CIA wakaanza kuhisi labda kijana huyu kweli hakuwa na hatia yoyote. Lakini kabla hawajalipa nafasi wazo hilo kukua kwenye vichwa vyao, wakaakua wafanye kitu cha kubahatisha, wakaingiza alama za vidole za kijana huyo katika mfumo wa kiusalama wa nchini kwao marekani na matokea ambayo waliyapata hakuna ambaye aliweza kuamini.

Kumbukumbu za mifumo ya kiusalama ya nchi za marekani zilionyesha kuwa mtu mwenye alama hizo za vidole zinafanana kabisa na mtu ambaye alijaribu kuingia nchini marekani siku ya tarehe 3 Agosti 2001 katika uwanja wa ndege wa Orlando, Florida akitokea Dubai. 

Maafisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wakamkataa kuingia nchini marekani kutokana na sababu kadhaa. Kwanza kijana huyo alikuwa na fedha dola 2,800 pekee na hii iliwapa shida maafisa wa uhamiaji kuelewa angewezaje kuishi nchini marekani? Pili kijana huyu alikuwa amekata tiketi ta kwenda pekee (one way ticket). 

Sababu hizi mbili zilipelekea maafisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege kuhisi kijana huyu alikuwa na mpango wa kuwa muhamiaji haramu kwani dalili hizo zilionesha kuwa hakuwa na mpango wa kurudi tena kwao. Hivyo basi maafisa hao wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wa Orlando wakamkataa kijana huyo juingia nchini marekani na wakamrudisha alikotokea.

Maafisa wa CIA walishitushwa na jambo hili na wakawasiliana na vyombo vingine vya usalama nchini Marekani na pasipo kupoteza muda maafisa kutoka shirika la upelelezi la FBI wakafika katika uwanja wa ndege wa Orlando, Florida ili wapate taarifa zaidi kuhusu nini hasa kilitokea siku ya Agosti 3 2001 siku ambayo kijana huyo alikataliwa kuingia nchini marekani.

Baada ya FBI kufika uwanja wa ndege waliomba kuzungumza na maafisa uhamiaji waliokuwepo siku ya tarehe 3 Agosti pia waliomba wapatiwe mikanda ya video ya kamera za ulinzi za uwanja wa ndege.

Baada ya kuangalia mikanda hiyo ya video, FBI waligundua jambo kubwa zaidi ambalo hawakulitegemea kabisa. Kamera za ulinzi zilizo nje ya uwanja zilirekodi gari inayomilikiwa na Mohamed Atta likiwa limepaki nje ya uwanja wa ndege.

Kwa wasiomfahamu Mohammed Atta ndiye alikuwa mtekaji kiongozi wa watu walioteka ndege za kimarekani na kwenda kuzigongesha katika magorofa ya WTC siku ya tarehe 11, Septemba 2001. Pia ndiye aliyeendesha moja wapo ya ndege hizo zilizotekwa.

Kwahiyo FBI wakang'amua kuwa siku hiyo Mohammed Atta alifika uwanja wa ndege kumpokea kijana huyo lakini kwa bahati mbaya maafisa uhamiaji walimkataa asiingie Marekani.

Hii ilikuwa na maana kwamba kama kijana huyu asingelitiliwa shaka na maafisa wa uhamiaji basi alitakiwa kuwa mojawapo ya washiriki walioteka ndege na kuzilipua katika majengo ya WTC siku ya Septemba 11, 2001.

Taarifa hizi ziliishitua FBI na pasipo kuchelewa wakawataarifu maafisa wa CIA katika jela ya siri nchini Poland ambako kijana huyu alikuwa anashikiliwa, na baada ya maafisa hawa kupata taarifa hii mara moja wakawasiliana na Makao Makuu ya CIA Langley, Virginia nchini Marekani.

Mara baada ya taarifa hizi kufika Makao Makuu ya CIA, Mkurugenzi wa CIA Bw. Leon Panetta akaamuru kijana huyo awekwe 'mahali salama' kwa ajili ya 'mahojiano' zaidi.

Ndege ikaandaliwa na safari ya kuelekea gereza la Guantanamo Bay ikaanza.

Jina halisi la kijana huyu anaitwa Mohammed al-Qahtani kipindi anakatwa alikuwa na umri wa miaka 21 na kwa sasa ana miaka 36 na ni mfungwa namba 63 (ISN 10063) katika gereza la Guantanamo Bay.

NDANI YA GUANTANAMO: 'MAHOJIANO' ZAIDI

Baada ya kijana al-qahtani kufikishwa katika gereza Guantanamo ambapo aliwekwa selo katika jengo lililoitwa Camp Delta 'mahojiano' zaidi yakaendelea. Licha ya mambo yote ambayo vyombo vya usalama viligundua juu yake lakini kijana yule aliendelea Kushikilia msimamo wake kuwa alikuwa anawinda kwenye milima ya Tora Bora.

Ilifikia hatua mpaka Katibu mkuu kiongozi wa makamu wa rais wa kipindi hicho Bw. David Addington pamoja na mshauri wa ikulu Bw. Alberto Gonzales walifika binafsi katika jengo la Camp Delta ndani ya gereza la Guantanamo mahsusi kwaajili ya kuongea na kijana al-qatani ili aeleze ukweli lakini kijana huyo akashikilia msimamo kuwa yeye ni muwindaji.

Ndipo hapa ilipofikia hatua hii Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa wakati huo akaidhinisha 'Mbinu za Mahojiano Zilizoboreshwa' (Enhanced Interrogation Techniques) zitumike kumuhoji kijana huyo. 

Mbinu hizi zilizoboreshwa zilikuwa zinajumuisha kwa mfano kutesa mfungwa kwa kumnyima pumzi kimateso kwa kumiminia maji (waterboarding), mikao ya msongo (stress positions), kumnyima usingizi n.k.

Uamuzi huu ulikuja kuleta mushkeli na watu wa haki za binadamu miaka iliyofuata.

Baada ya maafisa waliokuwa wanamuhoji kupewa idhini ya kutumia 'mbinu zilizoboreshwa' inasemekana kwamba kijana al-Qahtani ndiye mmoja wa wafungwa wa Guantanamo waliovunja rekodi kwa kuhojiwa muda mrefu zaidi kwa 'mbinu zilizo boreshwa'. Inasemekana kijana al-Qahtani alihojiwa kwa siku 48 mfululizo!

Baada ya 'mahojiano ya kina' yaliyochukua siku 48 kwa kutumia 'mbinu zilizoboreshwa' hatimae al-Qahtani akafunguka na kueleza ukweli.
Kwanza akakiri kuwa jina lake ni Mohammed al-Qahtani na ni raia wa Saudi Arabia. 

Pia akakiri kuwa ni yeye ndiye aliyekataliwa kuingia nchini Marekani siku ya Tarehe 3, Agosti 2001 na akaeleza kuwa alipewa maagizo na mtu anayeitwa Khalid Sheikh Mohammed ili aje marekani kwaajili ya kazi maalumu. Pia alieleza kuwa aliwahi kupatiwa mafunzo maalumu ya utendaji wa kishushushu na mawasiliano ya usiri (Operational training in Covert Communications) na aliyempatia mafunzo hayo alijulikana kama Abu Ahmed al-Kuwait.

Baada ya kupewa maelezo haya ilikuwa ni hatua kubwa kiasi kwa CIA lakini bado kulikuwa na mambo kadhaa hayakuwa sawia.

Kwa upande Khalid Sheikh Mohammed (KSM) mtu ambaye kijana huyu alimtaja kuwa ndiye alyemuagiza aje Marekani, mtu huyu alikuwa anafahamika vizuri na CIA. Walimfahamu kuwa ndiye moja wa Lutenati wa ngazi za juu wa kikundi cha Al Qaeda na ndiye 'mchora ramani' wa mashambulizi ya septemba 11, 2001.

Lakini mtu wa pili (Abu Ahmed al-Kuwait) aliyetajwa na huyu kijana kuwa ndiye aliyempatia mafunzo kijana juu ya ushushushu na mawasiliano ya siri, mtu huyu CIA walikuwa hawamfahamu. Ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kulisikia jina hilo. 

Hivyo basi kipaumbele kikawekwa kwamba kijana huyu 'ahojiwe' zaidi ili atoe taarifa zitakazofanikisha kumpata KSM (Khalid Sheikh Mohammed) 'mchora ramani' wa mashambulizi ya Septemba 11. Mahojiano kwa kutumia mbinu zilizobordshwa yakaendelea.

Kwa msaada wa maelezo waliyoyapata kutoka kwa kijana al-Qahtani maafisa wa CIA kwa kushirikiana na maafisa wa ISI (Inter-Service Intelligence - Idara kuu ya masuala ya usalama na ushushushu nchini Pakistani) walifanya oparesheni maalumu ya kumkamata KSM (Khalid Sheikh Mohammed) baada ya kumuwinda kwa muda mrefu sana na hatimae siku ya Machi 1, 2003 walifanikiwa kumkamata KSM akiwa hai katika katika jimbo la Ralwapindi nchini Pakistani. 

Baada ya kukamatwa tu na taarifa hiyo kufika makao makuu ya CIA Langley, Mkurugenzi mkuu Bw. Panetta akaamuru KSM awekwe 'mahali salama' mara moja. Na pasipo kupoteza muda siku hiyo hiyo CIA wakampandisha ndege KSM na kumpeleka gereza la Guantanamo. Na baada ya KSM kupokelewa Guantanamo alipewa selo kwenye jengo mojawapo la Guantanamo linaloitwa Camp Echo na akatambulika kama mfungwa namba ISN 10024.

Kesho yake 'mahojiano ya kina' yakaanza kwa kutumia 'mbinu zilizoboreshwa'.

Haikuchukua siku nyingi za 'mahojiano' KSM akaanza kufunguka na kusema ukweli. Kwanza akakiri kuwa yeye ndiye 'mchora ramani' wa shambulizi la Septemba 11, na ni moja ya malutenati wanaotegemewa na Al Qaeda katika kueneza propaganda za kikundi hicho. Akakiri kuhusika kutafuta vijana watakaotekeleza shambulizi hilo, akakiri kusaidia baadhi yao kupata mafunzo ya urubani na akakiri kusaidia kuwaingiza marekani vijana hao.

Maafisa wa jeshi na CIA walimbana zaidi KSM aeleze ni namna gani wanaweza kuwapata viongozi wa ngazi za juu wa Al-Qaeda na hasa hasa kiongozi mkuu lakini jibu la KSM liliwashangaza kila mtu. KSM akawaeleza kuwa hata yeye afahamu kiongozi mkuu yuko wapi au anapatikanaje. 

Mwanzoni walihisi anawadanganya lakini baada ya 'kumbana' zaidi wakagundua kuwa anamaanisha kuwa hajui 'kiongozi mkuu' yuko wapi wala namna ya kumpata.

KSM akawaeleza kuwa kiongozi mkuu, Osama Bin Laden aliacha kutumia simu toka mwaka 1998 maada ya mawasiliano yake ya simu ya satelaiti kudukuliwa na CIA na kuponea chupu chupu kuuwawa na wanajeshi wa kimarekani. 

Akawaeleza kuwa tangu hapo aliacha kutumia na mawasiliano ya simu na mawasiliano yote mengine ya kisasa na kwa upande wa mawasiliano akawa muumini wa falsafa ambayo imekuja kutumiwa na karibia maafisa wote wa ngazi za juu wa vikundi vya wapiganaji katika mashariki ya kati, kwamba; "If you live like you are in the 'past', the 'future' will never find you"! (Ukiishi kama upo kwenye nyakati za zamani, usasa hautakukamata kamwe).

Kwa hiyo mawasiliano yote yalikuwa yanafanyika kwa mdomo kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu au kwa barua za kuandika kwa mkono.

CIA wakambana zaidi aeleze je yeye alikuwa anapataje maagizo kutoka kwa kiongozi mkuu na akawajibu kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa anaaminika kwa asilimia mia moja na kingozi mkuu na ndiye aliyekuwa 'mpambe' wa karibu wa Bin Laden na kwamba kwa miaka kadhaa wapiganaji wa Al-Qaeda wala malutenati wa ngazi za juu walikuwa hawajawahi kumuona Bin Laden wala hawajui alipo na maagizo yote waliyapata kwa mdomo kutoka kwa mtu mmoja pekee aliyeitwa Abu Ahmed al-Kuwait.

Maafisa wote wa jeshi na CIA waliduwaa. Hii ilikuwa ni mara ya pili wanasikia jina hili. Mara ya kwanza walilisikia kutoka kwa kijana al-Qahtani kuwa alipatiwa mafunzo ya ushushushu na Abuu Ahmed al-Qahtani na sasa wanaelezwa na KSM ambaye ni lutenati wa ngazi za juu kabisa wa Al Qaeda kuwa hajawahi kumuona kiongozi mkuu kwa miaka kadhaa na maagizo yote yalikuwa yanaletwa kwake na mtu anayeitwa Abu Ahmed al-Kuwait. 

Kitu kilichowasahangza zaidi CIA ni kwamba walikuwa wanawafahamu viongozi na malutenati wote wa ngazi za juu wa Al Qaeda lakini jina hili lilikuwa jipya kwao. Hawakuwahi kumsikia Abu Ahmed al-Kuwait.

Wakiwa bado wapo kwenye mshangao wapigani wa kikurdi kutoka nchini Iraq wakawasiliana na serikali ya marekani kuwaeleza kuwa wamemkamata Hasaan Ghul moja ya mawakala wa Al Qaeda anayetegemewa nchini Iraq.
CIA wakampakia Hassan Ghul kwenye ndege na kumpeleka kwenye jela za siri nchini Romania. 

Baada ya 'kumuhoji' kwa siku kadhaa Hassan Ghul akawaeleza kuwa maagizo yote kuhusu mashambulizi na mipango mingine anayapata kutoka kwa kiongozi mkuu Osama Bin Laden kupitia kwa mtu anayemfahamu kwa jina la Abu Ahmed al-Kuwait.

Mshangao wa CIA ukageuka kuwa kitendawili. Huyu Abu Ahmed al-Kuwait ni nani na wanawezaje kumpata?

Mkurugenzi Mkuu wa CIA akaamuru kuwa kumtambua na kumkamata Abu Ahmed al-Kuwait kiwe kipaumbele namba moja..

Baada ya mchakato wa muda mrefu hatimae mwaka 2007 CIA walifanikiwa kumtambua Abu Ahmed al-Kuwait ni nani! Wakafanikiwa kupata jina lake halisi (Ibrahim Saeed Ahmed) na kwamba mwanzoni alikuwa ni mwanafunzi wa KSM kabla hajapanda ngazi kuwa mpambe wa Bin Laden.

Baada ya kumfahamu kwa kiasi CIA wakaanzisha mpango maalum wa kumchunguza ili wapate taarifa zaidi juu yake. Ili waweze kumpata kirahisi CIA wakafanya zoezi maalum la kuwatambua ndugu zake mbali mbali waliokuwa wanaishi kwenye nchi tofauti tofauti za kiarabu. 

Baada ya kuwatambua ndugu hao CIA wakafanya kazi ya kudukua mawasiliano ya simu ya ndugu zake na katika kitu kimojawapo ambacho walikigundua ni kwamba ndugu zake hao walikuwa na desturi ya kuwasiliana na namba za simu tofauti tofauti lakini zote zikiwa ni za Pakistan. Hii ilipelekea CIA kuhisi kwamba namba hizi ni za al-Kuwait lakini alikuwa anazibadilisha mara kwa mara ili kuepuka kugundulika.

Kwahiyo walichofanya CIA ni kusubiri siku ambayo ndugu yoyote wa al-Kuwait akipiga simu yoyote kwenda nchi ya Pakistan basi wataifuatilia namba hiyo ili wafahamu ni nani aliyekuwa anaongea naye.

Siku hiyo haikukawia sana kwani mwaka 2010 ndugu mmoja wapo alipiga simu kwenda Pakistan katika mji wa Pashwar. Kwa kutumia Wapalestina waliokuwa wanafanya kazi kwaajili ya CIA waliifuatilia simu hiyo mjini Pashwar na kuthibitisha kuwa aliyekuwa anaongea na simu hiyo alikuwa ni Abu Ahmed al-Kuwait. Baada ya al-Kuwait kumaliza kuongea na simu aliingia ndani ya gari na kuondoka na wapelelezi hao wakamfutilia kwa makini wajue anakoelea.

Pasipo kujua kuwa anafuatiliwa al-Kuwait aliendeshe gari mpaka mji wa Abbottabad. Na alipofika Abbottabad akaingia kwenye Jumba moja la kifahari. Jumba hili lilikuwa na muonekano na ulinzi uliotia shaka. Na hii ikapelekea CIA kuamini kuwa ndani ya jumba hilo hakuwa al-Kuwait pekee anayeishi bali kuna uwezekano mtu wa hadhi ya juu zaidi alikuwa anaishi humo ndani. Pengine labda kiongozi mkuu wa Al Qaeda, Osama bin Laden labda alikuwa ni mkazi humo ndani.

Waziristan Haveli

Baada ya CIA kugundua nyumba hii na kuitilia mashaka kuwa kuna uwezekano inamuhifadhi kiongozi wa hadhi ya juu wa Al Qaeda pengine labda Osama bin laden mwenyewe, hivyo wakaingiza wapelelezi katika mji wa Abbottabad ambao walinunua nyumba mjini hapo kama raia mwingine wa kawaida. Baada ya wapelelezi hao kufanikiwa kufanya mkazi mjini Abbottabad wakaanza kazi ya kukusanya taarifa juu ya jumba hilo na wakazi wake.

Wapelelezi hao ambao walikuwa ni raia wa Pakistan wanaofanya kazi kwa niaba ya CIA wakaanza kuwadodosa majirani na wakafanikiwa kupata taarifa za kutosha kiasi.

Kwanza majirani waliwaeleza kuwa jumba hilo linamilikiwa na mtu wanayemfahamu kama Arshad Khan (Abu Ahmed al-Kuwait) ambaye anaishi na kaka yake pamoja na familia zao. Majirani wakaeleza kuwa Arshad amewaeleza kuwa kuwa yeye ni msimamizi wa biashara za Hoteli za familia yao zilizopo Dubai. Pia majirani walimueleza kuwa Arshad (al-Kuwait) alikuwa ni 'mtu wa watu' na alikuwa anahudhuria karibia kila msiba mtaani kwao. 

Pia walielezwa kuwa licha ya kuwa na uwezo wa kifedha huwa anapenda kufanya manunuzi ya mahitaji yake ya nyumbani hapo hapo mtaani na mara kwa mara hutoka na watoto wake kwenda kuwanunulia mikate kwenye duka la uokaji (bakery) mtaani hapo.

Pia majirani waliwaeleza kuwa wamezoea kuliita jumba hilo Waziristan Haveli (Waziristan Mansion (Kasri la Waziristan)) kwani waliamini kuwa wakazi wa jumba hilo wanatokea Waziristan.

Baada ya CIA kupata taarifa hizi kutoka kwa wapelelezi waliojipenyeza mtaani hapo wakaamua wapanue wigo zaidi kwa kuwahusisha kitengo Maalumu cha Taifa la Marekani chini ya wizara ya ulinzi (DOD) kinachohusika na kukusanya taarifa na Ushushushu wa kijiografia (National Geospatial-Inttelligence Agency - NGA) ili wafahamu nukta baada ya nukta ya jumba hilo.

Kwa kutumia picha za satelaiti na kukusanya picha kwa kutumia ndege inayojiendesha yenyewe (drone) NGA walipata taarifa zote muhimu kuhusu jumba hilo kuziwasilisha CIA.

Taarifa yao ilieleza kuwa jumba hilo lililoitwa Waziristan Haveli lipo umbali wa takribani kilomita moja na nusu kutoka kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Abbottabad cha jeshi la Pakistan. Mtaani ambao jumba hili lilikuwepo ulikuwa na makazi ya wastaafu wengi wa jeshi la Pakistan.

Jumba hili lilichukua eneo kubwa zaidi kuliko nyumba nyingene za jirani kwani jumba lilijengwa kwenye eneo la ardhi lenye ukubwa la takribani mita za mraba 3,500.

Jumba hili lilizungukwa na ukuta wenye urefu wa futi 12 lakini ndani yake ukiingia unakutana na eneo la wazi tupu alafu anakuta ukuta mwingine wenye urefu wa futi 18. Kuta zoto hizi juu yake zilikuwa na waya za miba miba na umeme.

Pia jumba hili lilikuwa na ghorofa tatu na katika balkoni ya gorofa ya tatu ilikuwa na ukuta wake wa kuikinga wenye urefu wa futi 7. Pia kulikuwa na kamera za ulinzi katika kila kona ya jumba hili.

Pamoja na hayo pia NGA waligundua kuwa ndani ya jumba hilo kulikuwa na bustani kubwa iliyopandwa mboga mboga, pia kulikuwa na kuku zaidi ya 100, sungura pamoja na ng'ombe mmoja.

Pia jumba hili lilikuwa na mdirisha madogo na machache kiasi kwamba ukiliangalia haraka haraka unaweza kudhani halina madirisha kabisa.

Pia idara ya ushushushu wa kijiografia ya Marekani NGA ilifanikiwa kukusanya taarifa za wakazi wa jumba hilo ambapo walifanikiwa kung'amua kuwa Kasri hilo lilikuwa na wakazi wapata 22 wanaoishi ndani yake wengi wao wakiwa ni watoto. Pa waling'amua kuwa kulikuwa na takribani wakazi watani ambao kamwe walikuwa hawatoki nje ya jumba hilo.

Baada ya NGA kuwasilisha taarifa yao kwa CIA kuhusu vile walivyovibaini kuhusu jumba hili, Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Leon Panetta alizidi kushawishika kuwa Kasri hili lilikuwa linamuhifadhi kiongozi wa hadhi ya juu wa Al Qaeda na pengine ni Bin Laden mwenyewe anaishi humo.
Hivyo basi akaamuru ufanyike uthibitisho wa mwisho kuhakiki kama ni kweli kile anachokihisi.









No comments:

Post a Comment

SIXBERTY MANSON POSTS

Mona Lisa

  MONALISA                              LA GIOCONDA                          By Sixberty Manson  A picture by Sixberty Manson  MEET THE REAL...

ZILIZOTAZAMWA ZAIDI