MAANA YANGU
WRITTEN BY SIXBERTY MANSON
Ana Andika Sixberty Manson 👇
Kuna watu wanatukana Wazazi wao ila kuna wengine wanaisaka nafasi ya kuomba msamaha kwa Wazazi ila bahati mbaya wameshatangulia mbele za haki
Kuna Watu wanapanga mipango ya kuruka ukuta wa nyumbani kwao ili waende disco na viwanja ila kuna watu wanajaribu hata kupanda juu ya mabodi ya magari wajihifadhi usiku huu
Kuna watu wapo kwenye gari wanamwambia Baba au Mama aongeze kaubaridi ka AC, ila kuna watoto wanatembea wamejifunika sahani ya ndizi dhidi ya jua kali la Mjini
Kuna muda hutopigiwa simu, hautojuliwa hali na wala hata ukiumwa hutosaidiwa ila utakapofariki watatoa michango, watatoa magari, watajaza mafuta na watakupost status, watakuweka profile ingali haina maana tena
Kuna watu wanafungua maduka kwa ufahari ili waoneshe Jamii wana uwezo na wana nafasi ila kuna watu wanatembeza ndizi na machungwa wapate angalau pesa ya dawa na chakula
Kuna watu wana mijengo ya maana na Matajiri wa kutupwa ila hawana usingizi mizuri chini ya paa za nyumba zao, kula watu wana usingizi mzito ila hawana pakulala zaidi ya chini ya madaraja au nje ya frame za maduka
Kuna watu wapo ICU pale Muhimbili na mirija kila sehemu wakipambania uhai wao ila kuna watu wanajitia kitanzi au wanameza dawa kujiondoa uhai wao kisa Mapenzi, kisa moyo wa mtoto wa Mtu
Kuna wakati nimejifunza kupitia masherehe, kuna wale wenye mialiko mingi na hawana nafasi ya kwenda na wale wenye nafasi hawana hata hiyo mialiko zaidi ya kuhesabu status
Kwenye haki hakuna haki zaidi ya ushindi, Mwenye haki ya kweli hana Wakili wa viwango kutetea ukweli mwenye pesa hana haki ila ana pesa ya kumudu Wakili wa kweli, haki itatendeka kweli?
Yule unaemtegemea wala hakuamini, yule unaemuamini wala hakutaki
Maana yangu ni kuwa, kwenye hii dunia kila mtu anapigana vita ambayo hatujui chanzo chake ni nini, tuishi kwa kusaidiana na kuvumiliana
Asantee naitwa sixberty manson
No comments:
Post a Comment