Translate

Wednesday, March 4, 2020

USALITI WA NDOA

MPENZI  msomaji wangu Naitwa sixberty Manson 
karibu katika safu  ya saikolojia leo, kasi ya kusalitiana kwa wapenzi(wanandoa) wengi siku hizi imekuwa ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa na hii ni sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao. Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katika shida na raha siku zote. 

wapenzi waliogombana
Utafit wa wanasaikolojia umebani uhaminifu,nin silaha kubwa kwa wanandoa (wapenzi), mbali na mila ,tamaduni katika nchi au jamiina mengine.

Lakini hivyo hivyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine. Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wanandoa(wapenzi) wanachepuka? suluhu, hiki ndicho nilichopanga kuzungumzia siku  leo. Kwa wanandoa(wapenzi)  nitaainisha baadhi ya mambo ambayo kwa uchunguzi wangu nimebaini ndiyo yanayochangia kuchepuka kwa  wanandoa (wapenzi) walio wengi kuchepuka, wawe wako kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida.


sababu ni hizi;

TAMAA ZA KIMWILI NA PESA 
Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na kumhakikishia kwamba atampatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea. Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti.

Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.
TABIA ZISIZORIDHISHA 

Hapa wapo  wale  ambao wanaishi  maisha  ya  ajabu  sana, yaani wanaishi  katika(ndani) ya  ndoa  ama  wapo ndani ya uhusiano  wakielekea kwenye kuoana lakini  hawaaminiani  kabisa,  kila mtu anakuwa  na wasiwasi  juu ya mwenzake.     Afadhali  sasa  iwe kutokuaminiana  tu  lakini hapa  wapenzi  wanakuwa  hawasalitiani. 
Kuna wale ambao  ni  wazi  hawatulii  katika  mahusiano yao, yaani matendo yao (tabia)  tu  yanaonesha  dhahiri kabisa  kwamba, uaminifu  ni sifuri. Kuwa  kari bu sana  na  watu  wa  jinsia tofauti na  tabia ya kuwa na mawasiliano nao ya siri au mwanamke anapomuwekea  mumewe  vikwazo  katika  tendo la ndoa  chumbani (sex) anatarajia  akafanye wapi  na nani?  Kama  siyo kumwambia akatafute   wengine nje?    Hii ndiyo maana  wapenzi wenye tabia wanaowanyima  unyumba waume zao hata wanaposikia  kwamba  wanasalitiwa  wanakuwa hawana  nguvu ya kuwashutumu wapenzi wao, utamshutumuje wakati wewe humtimizii  katika mambo flani? Si hivyo tu, kwa upandea wa wanaume  nao  (baadhi )wengine wamekuwa  wakiwasusa  wake zao na kukaa  siku mbili au wiki na  zaidi  bila kuonekana nyumbani  hata kama atarudi nyumbani  basi  usiku  wa manane akiwa amelewa nawew  hana  mpango kabisa wa mapenzi  na mke wake,katika mazingira hayo  unadhani  nini  kinaweza kutokea kama siyo mwanamke kutafuta mwanaume atakayempatia mapenzi? Na mume kuoa mkee mwengine .
KUWEPO  KWA MAPENZI YA KILAGHAI
(uonngo).
Tunapozungumzia  mapenzi  tunaweza  kuyagawanya  katika makundi mawili, mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Walio katika  mahusiani au mapenzi ya kweli huwezi  kuwasikia wamesalitiana. Ila wale walio katika mapenzi ya kudanganyana tabia ya kusalitiana  ni  kitu cha kawaida  kwao na hivyo  kujikuta kila siku wakifumaniana.
UDHAIFU  KWA WAPENZI 

Udhaifu  ambao umezungumziwa  hapa  ni  ule  wa kimaumbile (big dick) ambao hata hivyo na wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza  kwamba, haiwezi kuchukuliwa kama ni miongoni  mwa  sababu  ya  kumsaliti  mpenzi wako uliyempenda kwa dhati. Kwa mfano, mwanaume unakuwa ‘Functionless’ yaani jogoo hawiki (tatizo ambalo si la kujitakia)  na  mke wake  hayuko tayari kuendelea  kuwa  naye  hivyo kulazimika  kuomba  talaka.  Lakini mwanaume anakuwa  mgumu  wa  kutoa  talaka  kutokana  na jinsi anavyompenda.

Wengi  wao wanachokifanya  ni  kuendelea  kuwa  katika  ndoa huku  wakiangalia uwezekano  wa kuanzisha au kuwa na  uhusiano  na  mtu  mwingine  wa  nje. Kwa wanawake  nao yawezekana kuwa  mwanamke hazai (tatizo  ambalo si la kujitakia pia na mwanaume anahitaji mtoto, atakachokifanya  ni kutoka(kuchepuka) nje ya ndoa yao  kwa siri lakini pia inaweza kufikia hatua mwanamke akagundua. Kwa  kifupi  ni kwamba ni c hanzo, kusalitiana kwa wanandoa  wengi  kumekuwa  kukitokea kutokana na  kuwepo  kwa mazingira fulani  ambayo  hupelekea kuwa  baadhi yao wamekuwa  wakishindwa  kujizuia nayo  na hivyo kujikuta  wanatoka  nje  ya mahusiano yao.

SULUHISHO
Ila sasa  na lazimika kwa nguvu zote  kuwashauri  wale  walio  katika  uhusiano wa kimapenzi, namaanisha  wapenzi wa kawaida, na  wachumba  pamoja  na wanandoa, tusiwe  na tamaa za kijinga na kufikia hatua ya kuwasaliti  wapenzi wetu. Hivi unajisikiaje unapomvulia  nguo  mtu  ambaye wala hana ‘future’ na wewe? Hivi  na wewe ukifanyiwa hivyo  na  mpenzi  wako  utajisikiaje? Sasa elewa yakuwa maumivu utakayoyapata  pale  utakaposikia mpenzi wako ana uhusiano  na  Fulani  ni hayohayo atakayoyasikia mwenza (mpenzi)  wako.
NI  kuwa  muaminifu, kuridhika  na unachokipata  kwake, muoneshe mapenzi ya dhati naye  atafanya hivyohivyo  na wote kujikuta  mnayafurahia  maisha yenu. Mfano, jadilini na kutatua matatizoyenu, kwa  pamoja  mipango  yenu ya familia, maendeleo, hali inayoleta mapenzi yenu  kuwa na furaha  na kulinda ndoa.

 

No comments:

Post a Comment

SIXBERTY MANSON POSTS

Mona Lisa

  MONALISA                              LA GIOCONDA                          By Sixberty Manson  A picture by Sixberty Manson  MEET THE REAL...

ZILIZOTAZAMWA ZAIDI